AL AHLY V SIMBA HAITAKUWA MECHI NYEPESI

    BAADA ya mchezo wa ufunguzi kufanyika Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa kinachofuata kwa sasa ni mchezo wa marudiano ugenini.

    Ipo wazi kwamba Simba, iliandika rekodi ya kuwa klabu ya kwanza ya Tanzania kucheza michuano mikubwa na mipya ya African Football League dhidi ya Al Ahly ya Misri.

    Haikuwa mechi nyepesi kutokana na ukubwa wa wapinzani Al Ahly ambao muda zote ni bora na mwisho kila mmoja alipata kile alichostahili baada ya dakika 90.

    Simba waliwahi kuwa wababe wa Ahly wanapocheza kwenye ardhi ya Tanzania lakini safari hii ilikuwa tofauti. Wengi walitarajia kuona Simba ikishinda ama Al Ahly kushinda haikuwa hivyo.

    Dakika 90 za mchezo, makosa ya kila timu yalitumika na wapinzani na mwisho wakatoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 kazi inafuata Misri.

    Kujipanga ni muhimu na kuamini kwamba wanauwezo wa kupata matokeo ugenini inawezekana kwa kuwa mpira unaduda na timu itakayojipanga na nafasi ya kupata matokoe chanya.

    Ahly haijawahi kuwa timu nyepesi na hasa inapocheza katika nchi yoyote barani Afrika, wao ndio wanakuwa ni wababe kwa kuwa ni klabu kubwa barani Afrika.

    Pamoja na hivyo, wanautambua ubora wa Simba na watajipanga na wanatambua wanatakiwa kuandika rekodi mpya kwa kuwa mashindano ya African Football League ni mapya na makubwa na rekodi zinatakiwa kutunzwa.

    Kazi kwenye mechi ya ufunguzi tayari ilishafungwa na sasa ni mechi ya pili ugenini. Makosa ya Simba hasa upande wa pembeni na mabeki ni muhimu kufanyiwa kazi kwa umakini kwenye mechi ya pili.

    Mchezo wa marudio unahitaiji mshindi na bahati mbaya Simba watakuwa ugenini.Rekodi ya kupoteza mechi za ugenini inawapa presha wengi hasa wakikumbuka kichapo cha mabao 5-0 walichowahi kupata Simba.

    Habari hizo zipo na rekodi hiyo ni mbaya kwa Simba ikiwa itaruhusu ijirudie. Inawezekana kupata matokeo ugenini lakini itakuwa kwa kazi kubwa kuanzia wachezaji kujituma na benchi la ufundi kuwa na chaguo bora kikosi cha kwanza.

    Pia inaweza kuwa tofauti kwa juwa hii ni football, mambo yanaweza kuwa tofauti kabisa na matarajio ya wengi na Simba akapoteza na kuondolewa kwenye mashindano haya kwa mara ya kwanza akiwa ugenini.

    Wachezaji wanapaswa kutambua huu ni mchezo wa maamuzi na sio mchezo wa ligi. Mshindi atakayepatikana hapa anasonga mbele hatua ya nusu fainali hivyo lazima watambue kazi yao haitakuwa nyepesi.

    Ipo wazi ugenini itabaki kuwa ugenini na Al Ahly hawatakubali kuona wanapoteza wakiwa nyumbani. Ni muda wa kujitoa kwa ajili ya kupata ushindi na kuulinda kwa kuwa kuna matatizo kwenye ulinzi pia kama ilivyotokea mechi iliyopita.

    Mashabiki wanapaswa kuelewa kwamba lolote kwenye mpira linaweza kutokea kwa kuwa dakika 90 zitaamua nani atakuwa nani ugenini. Wachezaji wana kazi kubwa kuwapa furaha mashabiki na Watanzania kiujumla.

    Muda ni sasa kwa ajili ya kupambana kupata matokeo ugenini na inawezekana kwa ajili ya kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.

    Kila la kheri wachezaji kwenye mchezo wenu na inabidi mtambue kwamba Al Ahly wanahitaji ushindi wakiwa mbele ya mashabiki zao.

    Kushindwa kupata matokeo kwenye mchezo wa nyumbani ni muda wa kujipanga kupata ushindi ugenini. Kila mmoja anaipa nafasi Al Ahly ya kushinda kutokana na uwekezaji hivyo wachezaji mnapaswa kuonyesha kwamba kila kitu kinawezekana.

    Previous articleNYOTA WA YANGA AIOMBEA DUA SIMBA DHIDI YA WAARABU
    Next articleAFL: AL AHLY 0-0 SIMBA