MAKOSA YAFANYIWE KAZI KUIMARISHA STARS

    DHAMIRA kubwa kwenye mechi za kirafiki ni kutambua makosa yalipo ili kuyafanyia kazi kwenye mechi zijazo. Tumeona namna wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania walivyopambana dhidi ya Sudan.

    Kupata sare ya kufungana bao 1-1 ugenini sio jambo la kujutia bali ni kuangalia wapi makosa yalifanyika. Kwenye safu ya ushambuliaji ni muhimu kuongeza umakini wakati ujao.

    Pia kuruhusu bao inaonyesha kwamba umakini kwenye safu ya ulinzi bado ni tatizo. Hapo ni muhimu kufanyia maboresho kwa wakati ujao kuwa imara zaidi. Muda ni sasa na inawezekana.

    Benchi la ufundi lina nafasi kubwa ya kufanyia kazi makosa hilo litakuwa ni muhimu kwa mechi zijazo. Kikubwa kwa wachezaji ni kuongeza umakini na nidhamu kwenye eneo la mazoezi.

    Umuhimu wa kushinda kwenye mechi zote ni muhimu katika kuongeza hali ya kujiamini kwa mechi zijazo. Kila mchezaji atakayepata nafasi ya kuwa katika timu ya taifa ni wajibu wake kutimiza majukumu.

    Muda ni sasa kuendelea kujituma na kupata matokeo chanya kwenye mechi za ushindani. Kila mmoja anawajibu wa kufanya tathimini kwa kile ambacho alionyesha kwenye mchezo husika.

    Mashabiki kazi yao ni kuendelea kuwa bega kwa bega na timu ya taifa kwa kuwa ni ya kila mmoja. Kikubwa ambacho kinapaswa kutokata tamaa kwa kuwa muda upo kwa ajili ya kufurahia mafanikio ya taifa.

     

    Previous articleHIVI NDIVYO MTU WA KAZI JOB ALIVYOMTULIZA CHE MALONE
    Next articleMALIZA JUMANNE YAKO VYEMA HUKU UKIPIGA MKWANJA NA MICHUANO YA EURO