Home Sports KAPOMBE AMEZIDISHA KAZI KAZI HUKO SIMBA

KAPOMBE AMEZIDISHA KAZI KAZI HUKO SIMBA

BEKI mkongwe ndani ya kikosi cha Simba, Shomari Kapombe amezidi kunoga kutokana na kasi yake ya kutoa pasi za mwisho za mabao ndani ya ligi.

Nyota huyo msimu wa 2022/23 alikuwa ni beki namba moja kwa waliotoa pasi nyingi za mwisho alipotoa nane kwenye mechi 25 alipokomba dakika 2,136.

Tayari kaanza kuonyesha kazi kwenye mechi za ligi alipofungua ukurasa wake kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Uhuru.

Pasi yake ya pili alitoa kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Sokoine alipompa mshikaji wake Clatous Chama.

Beki huyo ni shuhuda wa timu ya Simba ikitunguliwa mabao matatu kwenye mechi nne ambazo walicheza kwenye ligi na leo wanatarajiwa kuvaana na Singida Fountain Gate, Uwanja wa Liti.

Previous articleGEITA GOLD WAPOTEZA MBELE YA YANGA
Next articleYANGA: LIGI BADO MBICHI KABISA