Home Sports YANGA KAMILI GADO KUWAKABILI WAPINZANI WAO KIMATAIFA

YANGA KAMILI GADO KUWAKABILI WAPINZANI WAO KIMATAIFA

KIUNGO mkabaji, Mganda, Khalid Aucho na mshambuliaji, Mzambia, Kennedy Musonda wote wa Yanga wamesema kuwa wapo fiti tayari kuwavaa wapinzani wao Al Merrikh ya nchini Sudan.

Timu hizo zitavaana katika mchezo wa marudiano wa kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa leo saa moja kamili usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Katika mchezo huo, Yanga wataingia kifua mbele wakiwa na mtaji wa ushindi wa mabao 2-0 walioupata ugenini Kigali, Rwanda ambao ulipigwa mchezo huo.

 Aucho aliwaambia mashabiki wa timu hiyo, waonane uwanjani watakapokwenda kuandika historia ya kufuzu hatua ya makundi.

Aucho amesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia mia moja, kilichobaki wao wachezaji kufanya kile ambacho wamefundishwa katika kiwanja cha mazoezi na kocha wao Miguel Gamondi.

“Tuonane Jumamosi mashabiki wa Yanga, tunapokwenda kuandika historia ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika msimu huu,” alisema Aucho.

Naye Musonda amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi, wakati timu inapokwenda kucheza mchezo huo wa marudiano dhidi ya Al Merrikh.

“Ninaamini mashabiki wataujaza uwanjani zaidi ya wale waliokuja kutusapoti tulipocheza mchezo wa kwanza, Rwanda kiukweli mashabiki wanajitoa kwa ajili yetu wachezaji.

“Sasa ni kazi kubwa tumeibakiza sisi wachezaji, kuhakikisha tunawapa furaha mashabiki wetu kwa ushindi mwingine mkubwa hapa nyumbani, kama wachezaji tunaahidi kuipambania timu yetu,” amesema Musonda.

Previous articleASTON VILA YAICHAPA BRIGHTON
Next articleGAMONDI APANGUA KIKOSI KIMATAIFA, HIKI HAPA