>

GAMONDI APANGUA KIKOSI KIMATAIFA, HIKI HAPA

OCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Al Merrikh kutakuwa na mabadiliko ya kikosi tofauti na kile ambacho kilicheza katika mchezo wa kwanza kule nchini Rwanda.

Yanga katika mchezo uliopita ambao ulifanyika nchini Rwanda wakiwa ugenini walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Kennedy Musonda na Clement Mzize.

Gamondi amesema kuwa: “Kutakuwa na mabadiliko kwenye kikosi changu tofauti na mchezo wa kwanza wa ugenini, lakini jambo hilo sio muhimu zaidi kwa kuwa ni jambo la kiufundi.

“Kwa sasa naamini tunachotakiwa kwenda kukifanya ni kuhakikisha kuwa tunashinda huu mchezo ili tuweze kutinga katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika.

“Ni furaha kwangu kama nitaifanikisha timu hii kubwa kufika katika hiyo hatua na wachezaji wameniahidi hilo kuwa wao tayari kwa mapambano na kuwa mashujaa wa timu.

“Mchezo bado haujaisha kwa kuwa tuna dakika nyingine 90 ngumu tukiwa nyumbani na tunatakiwa kucheza kwa kujituma zaidi kwa kuwa hatuwezi kutegea kisa tulipata ushindi tukiwa ugenini,” amesema kocha huyo

Kikosi cha Yanga  itaanza katika mchezo wa leo dhidi ya Al Merrikh namna hii:-Djigui Diarra, Yao Khouasi, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Lomalisa, Mudathir Yahya, Maxi Nzegeli, Khalid Aucho, Kenedy Musonda, Aziz Ki, Jesus Moloko.