>

TWIGA STARS KAZINI LEO AZAM COMPLEX

KUELEKEA katika mchezo wa kuwania kufuzu Mashindano ya Mataifa ya Kimataifa Wanawake, (WAFCON) unaotarajiwa kuchezwa leo, benchi la ufundi la Timu ya Taifa ya Tanzania, Twiga Stars limeweka wazi kuwa lipo tayari.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex likiwa ni jambo la taifa na hakutakuwa na kiingilio.

 Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Bakari Shime amesema kuwa kazi kubwa ipo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

“Maandalizi yapo vizuri wachezaji wanatambua umuhimu wa mchezo tunaamini tutafanya vizuri kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu.

“Tunawaheshimu wapinzani hivyo tahadhari zote muhimu tunaichukua ili kupata matokeo katika mchezo. Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Shime.

Toure Clement, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Coast alisema utakuwa ni mchezo mgumu lakini wapo tayari kupata matokeo mazuri.

Mwaka 2010 Tanzania ilifuzu WAFCON Kwa kuwatoa Eritrea Tanzania 8-1 Eritrea, Eritrea 3-3 Tanzania na jumla ikawa ni 11-4 leo ni zamu ya Ivory Coast.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza uliochezwa Ivory Coast Tanzania ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.