UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi malengo yao msimu huu ni kuweza kupambana na kufanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kupata matokeo mazuri na kuwa nafasi za juu.
Jana Septemba 21, Azam FC ilikomba pointi tatu mazima dhidi ya Singida Fountain Gate.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 2-1 Singida Fountain Gate huku bao la ushindi likiachikwa na Iddy Suleiman, (Nado) dakika ya 90.
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa wanaendelea na maandalizi kwa mechi zao za ligi kupata matokeo mazuri.
“Kwenye mechi zetu zijazo tunahitaji kupata matokeo mazuri hivyo maandalizi yanaendelea tunaamini tutafanya kazi nzuri.
“Benchi la ufundi linawapa mbinu wachezaji ili kuendeleza ushindani katika mashindano ambayo tupo, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”