Home Sports SIMBA KUSEPA BONGO MAPEMA KUWAWAHI WAZAMBIA

SIMBA KUSEPA BONGO MAPEMA KUWAWAHI WAZAMBIA

KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamo ya Zambia uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa utaondoka mapema kuwawahi wapinzani wao.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 16 ikiwa ni wa hatua ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu ya Simba inapeperusha bendera kwenye anga la kimataifa sawa na Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Singida Fountain Gate wao wakiwa kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Singida Fountain Gate wao watakuwa Azam Complex huku Yanga wao watakuwa Rwandakwenye msako wa ushindi katika mechi zao.

 Mratibu wa Simba SC, Abbas Ally ameweka wazi kuwa mpango wao ni kuanza safari mapema kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wakiwa Zambia.

“Timu itaondoka mapema Alhamisi kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Power Dynamo maandalizi yanakwenda sawa malengo ikiwa ni kuona kila kitu kinakwenda vizuri,”.

Previous articleYANGA WACHOREWA RAMANI YA USHINDI MBELE YA WAARABU
Next articleSIMBA NA YANGA MAKUNDI WEKENI HESABU ZA LAZIMA