Skip to content
AISHI Manula, kipa namba moja wa Simba amerejea rasmi uwanjani na kuanza mazoezi maalumu ili kurejea kwenye ubora wake.
Kipa huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Roberto Oliveira alipopata maumivu ni Ally Salim alikuwa mbadala wake.
Manula hakuwa kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi msimu wa 2022/23 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga na alihushudia Salim akianza.
Kwenye mchezo huo ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-0 Yanga huku Salim akiandika rekodi ya kukomba dakika 90 bila kutunguliwa kwenye mchezo huo.
Daktari wa Simba, Edwin Kagabo amesema kuwa maendeleo ya kipa huyo yanazidi kuwa bora.
“Manula anazidi kuimarika kwa asilimia kubwa kwa kuwa muda mrefu alikuwa nje na sasa amefikia hatua ya kuanza mazoezi maalumu kwenye eneo la uwanja.
“Hii ni kuangalia maendeleo yake ambayo kwa asilimia kubwa yanaridhisha,”.