TIMU HII YAPEWA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

KOCHA wa zamani wa Yanga, Nassredine Nabi amesema kuwa ameiangalia Yanga ya sasa chini ya Miguel Gamondi na kusema kuwa inauwezo mzuri wa kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Nabi kwa sasa ni kocha wa Far Rabat ya Morroco na msimu uliopita aliiongoza Yanga kuipa ubingwa wa ligi kuu, Kombe la FA Ngao ya Jamii na kufika fainali katika Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni rekodi kwa timu hiyo.

Akizungumza kuhusiana na uwezo wa Yanga kutwaa ubingwa msimu huu, Kocha Nabi alisema kuwa bado anaamini Yanga wana timu nzuri baada ya kuiangalia katika michezo kadhaa ambayo wamecheza mpaka sasa na kubaini kuwa bado wanakikosi imara.

Yanga bado wanatimu nzuri na tayari nimeona michezo kadhaa ambayo wamecheza, usajili ambao umefanyika ni mzuri na mara zote wamekuwa na machaguo sahihi, uongozi ulikuwa makini katika hilo.

“Ambacho kipo kwa sasa ni kwa kocha kuona namna gani ataweza kuwatumia wachezaji na kupata matokeo, kuwaunganisha vyema na kujua jinsi ya kuwatumia katika michezo husika,” amesema kocha huyo.