Home Sports SIMBA YAREJEA KAMBINI KUIVUTIA KASI POWER DYNAMO

SIMBA YAREJEA KAMBINI KUIVUTIA KASI POWER DYNAMO

BAADA ya kukamilisha mechi mbili za Ligi Kuu Bara na kukomba pointi sita jumlajuma, tayari wachezaji wa Simba pamoja na benchi la ufundi wamerejea kambini.

Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa ligi ni Yanga chini ya kocha Miguel Gamondi.

Yanga imeanza kwa kasi msimu wa 2023/24 sawa na Simba ambao ni watani zao wa jadi wote wakishinda mechi zao za mwanzo.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Manungu, ubao ulisoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba na ule wa pili ubao wa Uwanja wa Uhuru ulisoma Simba 2-0 Dodoma Jiji.

Vinara wa ligi kwa sasa ni Yanga wakiwa na pointi sita tofauti ya mabao ya ufunga na kufungwa ambapo Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi imetupia mabao 10 kibindoni.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa baada ya mapumziko kikosi kimerejea kambini kwa maandalizi ya mechi za kimataifa.

“Mchezo wetu wa Dodoma Jiji ulipokamilika ni mapumziko wachezaji walipewa wapo ambao walibaki Dar na wengine walielekea mikoani kwa ajili ya mapumziko.

“Wachezaji wengine walikwenda nje ya Dar hilo lilikuwa ni muhimu kwao kwa kuwa walipewa mapumziko. Sasa wamerejea kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Power Dynamo ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika,”.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septema 16, Uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia.

Previous articleISHU YA PENALTI YAMVURUGA GAMONDI
Next articleTIMU HII YAPEWA UBINGWA WA LIGI KUU BARA