Home Sports ISHU YA PENALTI YAMVURUGA GAMONDI

ISHU YA PENALTI YAMVURUGA GAMONDI

ZAWAD Mauya, kiungo mzawa mkabaji ndani ya kikosi cha Yanga amekutana na kisanga kutoka kwa Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi baada ya kuwa chanzo cha penalti katika mchezo huo.

Ikumbukwe kwamba Yanga katika mechi tano mfululizo ilizocheza ilikuwa haijaruhusu bao la kufungwa rekodi hiyo ilitibuliwa na ASAS FC kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ni dakika ya 84 Mauya wa Yanga alisababisha penalti ikafungwa na Tito Mayor aliyempoteza mazima kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra na mwisho ubao ulisoma Yanga 5-1 Azam FC.

Gamondi ameweka wazi kuwa kufungwa kwa penalti ni jambo ambalo hakufikiria lakini kwa kuwa ni mchezo kuna kazi anakwenda kuifanya kwa wachezaji wote.

“Nilikuwa ninapenda kuona hatufungwi ila imetokea tumefungwa bao moja kwa penalti. Kwa kilichotokea ni makosa ya wachezaji hilo tunakwenda kulifanyia kazi kwenye eneo la mazoezi.

“Kitakachotufanya tuwe bora ni kufanyia kazi makosa yetu kwenye mechi. Kwa kuwa tuna muda nina amini tutakuwa imara na tutaendelea na kazi kwenye mechi nyingine,”.

Previous articleSIMBA YAFUNGUKIA KASI YA YANGA KWENYE LIGI KUU BARA
Next articleSIMBA YAREJEA KAMBINI KUIVUTIA KASI POWER DYNAMO