SIMBA YAFUNGUKIA KASI YA YANGA KWENYE LIGI KUU BARA

MASHABIKI wa Simba wamezungumzia kasi ya Yanga ambayo inakwenda nayo kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kupata ushindi wa mabao 5-0 JKT Tanzania. Yanga iliibuka na ushindi huo katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Huu unakuwa ni ushindi wa pili kwenye ligi Yanga kushinda mabao 5-0 ambapo timu ya kwanza kutunguliwa ilikuwa ni KMC mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.