Home Sports THANK YOU YA KWANZA KWA KOCHA BONGO

THANK YOU YA KWANZA KWA KOCHA BONGO

SINGIDA Fountain Gate imeweka wazi kuwa Hans Pluijm hataendelea kuwa kwenye benchi la ufundi msimu wa 2023/24.

Pluijm amepewa mkono asante Agosti 29 ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa sasa timu hiyo ya Singida Fountain Gate itakuwa chini ya Mathias Lule ambaye ni kocha msaidizi.

Mchezo wa mwisho kukaa benchi ilikuwa ni Agosti 27 katika mchezo wa kimataifa ubao ulisoma JKU 2-0 Singida Fountain Gate.

Licha ya kupoteza mchezo huo Singida Fountain Gate wametinga hatua inayofuata kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-3 kwa kuwa mchezo wa kwanza walipata ushindi wa mabao 4-1 Uwanja wa Azam Complex.

Hii inakuwa ni Thank You ya kwanza kwa kocha ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo imeanza kwa ushindani mkubwa katika mzunguko wa kwanza.

Previous articleNI MWENDO WA 5G, SIMBA YATAJA WANAOWAPA JEURI
Next articleSIMBA YAFUNGUKIA KASI YA YANGA KWENYE LIGI KUU BARA