Home Sports YANGA MWENDO WA 5 G KWENYE LIGI

YANGA MWENDO WA 5 G KWENYE LIGI

MWENDO wa 5G kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga kwa wapinzani wao unaendelea.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex umesoma Yanga 5-0 JKT Tanzania.

Kasi ya ufungaji kwa Yanga ilizidi kipindi cha pili yalipofungwa mabao manne na kipindi cha kwanza ilikuwa bao moja.

Aziz KI alifungua pazia dakika ya 45 kwa pigo la faulo kisha kipindi cha pili Kennedy Musonda alipachika bao dakika ya 54.

Yao Attouhula dakika ya 64 alizama nyavuni huku Maxi Nzengeli alipachika mabao mawili dakika ya 79 na 88.

Timu ya Kwanza kutunguliwa mabao matano ilikuwa KMC na Leo ni JKT Tanzania, Yanga inafikisha poiñti inaongoza Ligi.

Previous articleKOCHA SIMBA APEWA DAKIKA 180
Next articleMUDA ULIOBAKI KWA USAJILI UTUMIKE KWA UMAKINI