MUDA ULIOBAKI KWA USAJILI UTUMIKE KWA UMAKINI

HAKUNA marefu yasiyo na ncha ipo hivyo na ukweli hauwezi kuwekwa kando kwa namna yoyote lazima utakutana nao.

Sio Yanga, Simba hata Singida Fountain Gate ni muhimu kukamilisha utaratibu kwa wakati na umakini mkubwa.

Tumeona wapo makocha ambao wameanza na timu kwa mwendo wa kusuasua wana nafasi ya kufanya maboresho kwa wakati ujao.

Kwa wakati uliobaki kwenye dirisha la usajili ni kukamilisha ile mipango ambayo ilikuwa bado haijakamilika kwa timu husika.

Imani ni kwamba hakutakuwa na muda mwingine kukamilisha usajili ambao ulikuwa ni muhimu kwa timu zote Bongo.

Wapo wachezaji waliofanya vizuri na kupata timu na wapo ambao walishindwa kuendelea kuwa na timu zao kutokana na kushindwa kufanya kile kilichokuwa kinatarajiwa.

Ikumbukwe kuwa Agosti 31 dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa kwa timu zote.

Kwa wakati uliobaki wale ambao hawajakamilisha usajili wakati uliobaki utumike kwa umakini. Pia uwe ni muda wa mwendelezo kwa wachezaji kuongeza umakini kwa ajili ya wakati ujao.

Ipo wazi kuwa wale walioasajiliwa kwenye mechi za mwanzo kuna kitu kimeanza kuonekana katika mechi za kitaifa na kimataifa.

Muda uliobaki utumike kukamilisha yote kuwa imara na bora kwenye mechi zote. Kukamilisha usajili mapema kutaongeza nguvu ya kuendelea kufanya vizuri kwa mechi zijazo.

Zilizopanda daraja ikiwa ni Mashujaa na JKT Tanzania zinapaswa kutambua ushindani ni mkubwa mwanzo mwisho na zile ambazo zilishuka bado zina nafasi ya kurejea.