Home Sports KOCHA SIMBA APEWA DAKIKA 180

KOCHA SIMBA APEWA DAKIKA 180

BAADA ya kukiongoza kikosi cha Simba kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara kwa kukomba ushindi kwenye mechi zote mbili, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira amepewa dakika 180 za moto kimataifa.

Mechi ambazo Oliveira alikiongoza kikosi cha Simba ilikuwa ugeini ubao wa Uwanja wa Manungu ulisoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba na alikamilisha dakika 180 kwa kushuhudia ubao Uwanja wa Uhuru ukisoma Simba 2-0 Dodoma Jiji.

Ni kete mbili kimataifa katika hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo inatarajiwa kumenyana na Power Dynamo ya Zambia.

Kete ya kwanza kwa Simba itakuwa ugenini na mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 15-17 ugenini na ule wa marudiano ambao Simba watakuwa nyumani unatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 29- Oktoba Mosi.

Ni dakika 180 za moto kwa Oliveira ambaye anapambana kusaka kikosi cha kwanza cha ushindani kutokana na kuwa na maingizo mapya katika kikosi hicho na wale ambao walikuwa ndani ya kikosi kwa msimu wa 2022/23.

Kocha huyo amesema:, “Tuna wachezaji wazuri ambao tunaamini watatupa matokeo kwenye mechi zetu kikubwa ni kuona tunapata ushindi kwani Simba ni timu kubwa,”.

Previous articleSHEREHE KWA YANGA KISA KUWAFUNGA ASAS INATOSHA
Next articleYANGA MWENDO WA 5 G KWENYE LIGI