GAMONDI KWENYE VIATU VYA NABI

TARATIBU Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameanza kuwa kwenye viatu vya Nasreddine Nabi kutokana na mbinu zake kuwa kwenye mrandano wa Nasreddine Nabi aliyewahi kuwa kocha wa Yanga.

Nabi alikuwa imara kwenye mbinu za kubadili mchezo kwa kutumia wachezaji walioanza kusugua benchi na walipoingia waliwapa tabasamu mashabiki na wachezaji kiujumla.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa kimataifa zama za Nabi kwenye mchezo dhidi ya Club Africain ugenini ni Aziz KI alipachika bao hilo kwenye mchezo uliochezwa 9/11/2023 wakiwa ugenini.

Aziz KI alipachika bao hilo akitokea benchi ilikuwa zama za Nabi na ilikata tiketi ya kutinga hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Safari ilikwenda mpaka fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Chini ya Gamondi ngoma imeanza taratibu kujibu ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya ASAS Djibout uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Agosti 26.

Katika mchezo huo mastaa wawili wa Yanga waliingia wakitoekea benchi ikiwa ni Clement Mzize na Pacoume Zouzoua hawa wawili walifunga bao mojamoja kwenye mchezo huo.

Mwisho ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 5-1 ASAS Djibout na Yanga inasonga mbele katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika inatarajiwa kumenyana na Al Merrikh ya Sudan.