Home Sports AZAM FC YAIPIGA BAO YANGA KATIKA HILI

AZAM FC YAIPIGA BAO YANGA KATIKA HILI

WAKATI Yanga wakiwa katika kampeni ya kukaa katika nafasi ya kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara, Azam FC wameanza kujibu mapigo kwa kuishusha Simba.

Ushindi wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya Tanzania Prisons umewaongezea pointi tatu na kuwafanya wafikishe pointi sita kibindoni.

Mabao ya Prince Dube dakika ya 11, Idd Nado dakika ya 47 na Nathaniel Chilambo dakika ya 82 yalitosha kuwapa pointi tatu Azam FC Uwanja wa Azam Complex ambao unatumiwa pia na Yanga kwenye mechi za ushindani.

Bao pekee la Tanzania Prisons lilipachikwa na Zabona Khamis dakika ya 90+2 ikiwa ni dakika za lala salama.

Yanga leo ina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya JKT Tanzania mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Previous articleGAMONDI KWENYE VIATU VYA NABI
Next articleSHEREHE KWA YANGA KISA KUWAFUNGA ASAS INATOSHA