JKU SIO WA MCHEZOMCHEZO WAWAPA SOMO SINGIDA FOUNTAIN GATE

JKU SC waliwapa ushindani mkubwa Singida Fountain Gate katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ni mchezo wa pili uliochezwa Agosti 27 walishuhudia ubao ukisoma JKU 2-0 Singida Fountain Gate.

Ushindi wa JKU SC kwenye mchezo wa pili umeonyesha kuwa wapinzani hao hawakuwa wa mchezomchezo likiwa ni somo kwa Singida Fountain Gate kujipanga upya kwenye mechi zinazofuata kimataifa.

Ukuta wa Singida Fountain Gate umeonekana ukikwama kuongeza umakini kwenye ulinzi huku safu ya ushambuliaji nayo ikwama kutumia nafasi ambazo wanatengeneza.

Ni mabao ya Nassor Juma dakika ya 7 na Gamba Matiko dakika ya 42 yaliwapa ushindi JKU SC.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa kwanza uliochezwa Agosti 18 ubao ulisoma Singida Fountain Gate 4-1 JKU SC.

Katika mchezo huo nyota Marouf Tchakei alitupia kambani mabao mawili huku Morice Chukwu na Duke Abuya wakitupia bao mojamoja.

Singida Fountain Gate wanapenya hatua inayofuata kwa jumla ya ushindi wa mabao 3-4 ambapo watamenyana na Future ya Misri.