Home Sports PETER BANDA AKUTANA NA THANK YOU SIMBA

PETER BANDA AKUTANA NA THANK YOU SIMBA

KIUGO Peter Banda hatakuwa ndani ya kikosi cha Simba msimu wa 2023/24.

Usajili wa nyota huyo ulileta mtikisiko ambapo alikuwa anatajwa kupokwa airport na watani zao wa jadi Yanga jambo ambalo lilizua gumzo.

Mwisho Simba walimtambulisha ndani ya kikosi hicho na kuzima kele za watani wao wa jadi Yanga kushinda vita ya kuinasa saini ya nyota huyo.

Kiungo huyo raia wa Malawi msimu wa 2022/23 hakuwa na mwendo mzuri kutokana na kutokuwa fiti kwa muda mrefu alipokuwa akipambania afya yake.

Agosti 28 uongozi wa Simba umebainisha kuwa hautakuwa na kiungo huyo mwenye kipaji ndani ya Simba.

“Asante kwa muda wote uliokuwa sehemu ya familia ya Simba SC. Kila la kheri Peter Banda,” ilieleza taarifa hiyo.

Banda ni shuhuda wa Yanga wakitwaa ubingwa msimu wa 2022/23 kwenye Ligi Kuu Bara ambapo Simba iliambulia patupu.

Previous articleJKU SIO WA MCHEZOMCHEZO WAWAPA SOMO SINGIDA FOUNTAIN GATE
Next articleGAMONDI ATUMA UJUMBE HUU JKT TANZANIA