GAMONDI ATUMA UJUMBE HUU JKT TANZANIA

LICHA ya kwamba mchezo wa mwisho kabla ya JKT Tanzania kushuka daraja na Yanga kukomba pointi tatu bado mabingwa hao watetezi wameweka wazi kuwa wanawaheshimu wapinzani hao.

Kwenye mchezo wa mwisho kukutana na Yanga ubao ulisoma JKT Tanzania 0-2 Yanga na mabao yalifungwa na Yacouba Songne na Tuisila Kisinda.

Kesho Agosti 29 Yanga wanatarajiwa kumenyana na timu hiyo mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, saa 1:00 usiku.

Gamondi amesema: “Licha ya kwamba mpinzani wetu tunajua ni timu iliyopanda daraja, najua kwamba wana wachezaji wenye uzoefu kwenye ligi hivyo hatupaswi kuichukulia kama timu dhaifu au ngeni kwenye ligi.

“Ni wageni kwa maana ya timu lakini wana idadi kubwa ya wachezaji wenye uwezo lakini sisi ni timu kubwa na tupo nyuma nafikiri kesho tunapaswa kujiamini na kufunga magoli mengi,”.

Yanga mchezo huo unatarajiwa kuwa wa pili ambapo ule wa kwanza waliibuka na ushindi wa mabao 5-0 KMC.

Yanga ilindinka rekodi ya kuwa timu iliyoshinda ushindi mkubwa katika mzunguko wa kwanza msimu wa 2023/24.

Na rekodi zinaonyesha kuwa nyota wa kwanza kufunga bao ndani ya Yanga ni beki Dickson Job aliyefanya hivyo dakika ya 16.