Home International PANGA LINAPITA KWA WASHIKA BUNDUKI HUKO

PANGA LINAPITA KWA WASHIKA BUNDUKI HUKO

ARSENAL iko tayari kuwauza wachezaji tisa ili
wapate fedha kwa ajili ya kumpa nguvu Kocha
Mikel Arteta ya kushusha jembe lingine kikosini
hapo.

The Gunners wametumia mkwanja mkubwa
msimu huu wa joto ili kushindana kusaka
ubingwa wa Premier ambao msimu uliopita
waliukosa dakika za mwisho mbele ya
Manchester City.

Arsenal wametoa pauni 105m kwa Declan Rice,
pauni 65m kwa Kai Havertz na pauni 36.5m kwa Jurrien Timber, kwa matumaini wanaweza
kumaliza miongo miwili ya kusubiri taji la ligi.

Kufikia sasa, walioondoka kikosini hapo ni
nahodha wa zamani Granit Xhaka, aliyetua
Bayer Leverkusen kwa pauni milioni 21.4, huku mauzo ya Pablo Mari, Matt Turner na Auston
Trusty pia yakizidisha hazina.

Kocha Arteta anahitaji zaidi ya pauni milioni
100 ili kuendelea kuisuka timu yake na tayari
amewaruhusu wachezaji tisa kuwekwa sokoni.

Nyota hao waliopo sokoni ni Folarin Balogun,
Gabriel Magalhaes, Kieran Tierney, Takehiro
Tomiyasu, Albert Sambi Lokonga, Rob Holding,
Cedric Soares, Nicolas Pepe na Nuno Tavares
hivyo wanaweza kusepa kabla ya Septemba 1.

Previous articleBETO YA VIUNGO SIMBA NI PASUA KICHWA
Next articleGAMONDI ANASA FAILI LA AL MERRIKH