BENKI ya NMB Tanzania imeweka wazi kuwa sababu kubwa ya kuendelea kuwa karibu na Watanzania wengi zaidi wameamua kuendeleza mpango wao wa kudhamini mashindano ya Gofu Tanzania.
Taarifa kutoka NMB imeeleza kuwa kwa kutambua umuhimu wa michezo kwenye jamii, NMB inaendelea kuwa wadhamini wakuu wa mashindano ya Gofu ya Mkuu wa Majeshi kwa mwaka 2023.
Mashindano hayo kwa 2023 yanatarajiwa kufanyika Lugalo Golf Club, Septemba 2 na 3.
Huu unakuwa ni mwaka wa 8 kwa NMB kudhamini mashindano hayo, huku wakiwa na lengo la kuhakikisha wanawafikia Watanzania wengi zaidi kulingana na michezo wanayopenda.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi Aikansia Muro amekabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 30 kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo ikiwa ni udhamini wa mwaka huu.