MUDA WA MIPANGO NI SASA LIGI INAHITAJI NGUVU

    MUDA uliopo kwa sasa ni kwa ajili ya msimu mpya ambapo maandalizi yanapaswa kuwa endelevu kwa kila mchezo husika.

    Matokeo yanayopatikana uwanjani baada ya dakika 90 inatokana na kile ambacho wachezaji wameamua kukionyesha kwenye mchezo husika.

    Ni anga la kitaifa na kimataifa timu zina kazi ya kupambana kufanya vizuri kwa kuwa furaha inabebwa na matokeo ambayo yanapatikana uwanjani.

    Kuanza kwa msimu mpya inamaanisha kwamba hata yale malengo ambayo yalipangwa msimu uliopita nayo yanatakiwa kuboreshwa kuwa bora zaidi.

    Ikiwa timu iliandika malengo kuishia ndani ya 10 bora kisha ikashindwa ni muda wa kuangalia wapi malengo yao yalikwama kisha kupanga mpango kwa ajili ya kufikia mipango yao.

    Zipo timu ambazo mechi za kimataifa hazijapata matokeo na nyingine kwenye mechi za ligi pia huo sio mwisho wa mashindano kila hatua ni muhimu kuitazama kwa ukaribu.

    Iwe ni Mashujaa, Namungo FC, Ihefu, Kagera Sugar zote ni muhimu kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kupata matokeo.

    Hata Yanga ambao ni mabingwa watetezi kibarua chao ni kurejesha taji kwa mara nyingine na ipo wazi kwamba haitakuwa rahisi.

    Kwa wale ambao wapo kwenye mashindano ya kimataifa ni muhimu malengo yao kuyaweka wazi kwa wachezaji ili watambue kile kinachotakiwa kufanyika kwa mechi zinazofuata.

    Kwenye ligi pia hivyohivyo ni muhimu kuangalia mechi zilizopita makosa yalipokuwa na kujipanga upya kwa ajili ya mechi zinazofuata.

    Mzunguko wa kwanza unakuwa na ushindani mkubwa na ule wa pili pia ni hivyohivyo kikubwa kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni umakini na utulivu kwenye mechi zote za nyumbani na ugenini.

    Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa muhimu kufanya kweli na kupata matokeo mazuri.

    Previous articleWENYE LIGI TUMEANZA KAZI, BALEKE APEWA MABAO 30
    Next articleANAYECHEKA MWISHO HUYO HUCHEKA ZAIDI