Ligi Kuu ya nchini Saudi Arabia inayoitwa Roshn Saudi League imezidi kuongeza nguvu ya mastaa wenye majina baada ya kumvuta staa wa PSG ndani ya ligi hiyo.
Ni Klabu ya Al-Hilal rasmi imeinasa saini ya Mbrazil Neymar JR hivyo atakuwa kwenye timu hiyo msimu wa 2023/24.
Nyota huyo aliyeng’ara na PSG ya Ufaransa na Barcelona ya Hispania anaungana na Cristiano Ronaldo, Sadio Mane, Karim Benzema, N’Golo Kante, Roberto Firmino na wengine wengi ambao tayari ‘wanakiwasha’ nchini Saudi Arabia.
Nyota huyo ni mshikaji mkubwa wa staa Mbappe ambaye walikuwa naye pamoja ndani ya PSG.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)