Home International CAICEDO AIGOMEA LIVERPOOL, HUYO CHELSEA

CAICEDO AIGOMEA LIVERPOOL, HUYO CHELSEA

DILI la staa wa Brighton FC Moises Caicedo kuibukia Liverpool linaweza kubuma licha ya asilimia 99 kuwa upande wao.

Nyota huyo wa Brighton alikuwa katika mazungumzo na Liverpool ambao waliweka mkwanja mrefu mezani wa euro 110 milioni.

Jurgen Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool aliweka wazi kuwa kila kitu kuhusu Caicedo kipo tayari ni jambo la kusubiri tu.

Taarifa zimeeleza kuwa Caicedo amewaambia Liverpool kuwa anapenda kujiunga na Chelsea hivyo hatasafiri kwenda Liverpool na anaweza kutambulishwa muda wowote.

Previous articleMASHUJAA WAINGIA ANGA ZA SIMBA NA YANGA
Next articleHISTORIA IMEANDIKWA UDHAMINI WA NBC LIGI KUU BARA