WAKIWA wanajiandaa kuikabili Yanga mchezo wa Ngao ya Jamii nusu fainali, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga mastaa wa Azam FC, Prince Dube na Abdul Suleiman, ‘Sopu’ wameongezewa makali kumtungua Dijigui Diarra.
Azam FC ilikuwa Tunisia kwa kambi ya muda kuelekea msimu wa 2023/24 na tayari wamerejea Dar na kuanza maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao dhidi ya Yanga.
Ni Agosti 9 wanatarajiwa kuvuja jasho huku Kocha Mkuu wa Azam FC Youssouph Dabo akiweka wazi kuwa anawaongezea mbinu za kushambulia wapinzani wapinzani wao.
Miongoni mwa mastaa wa Azam FC ambao wapo kwenye maandalizi ya msimu mpya ni Sopu aliyemtungua mabao mawili kipa namba moja wa Yanga Djigui Diarra msimu wa 2022/23 kwenye mchezo wa ligi.
Mbali na Sopu yupo Prince Dube, Idris Mbombo ambao ni washambuliaji huku Yannick Bangala huyu ni kiraka akiwa pamoja na Feisal Salum waliokuwa pamoja ndani ya Yanga.
Dabo amesema: “Tunaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuimarisha kikosi ikiwa ni pamoja na eneo la ushambuliaji dhidi ya wapinzani wetu katika mchezo tunatambua kwamba kuna ugumu katika kuwabili wapinzani ila tunajitahidi,”.
Related News
Germany's defender #15 Nico Schlotterbeck celebrates after scoring his team's second goal during the 2026 World Cup Group E football match between Germany and Curacao at the Houston Stadium in Houston on June 14, 2026. (Photo by RONALDO SCHEMIDT / AFP)