MATESO LAZIMA YAGOTE MWISHO, MWANZO MPYA

    MATESO makubwa ambayo yanatokea kwa viongozi kushindwa kutimiza ahadi zao yanawatesa mpaka mashabiki kutokana na matokeo kuwa mabaya.

    Kwa yale ambayo yamepita msimu wa 2022/23 ni muda wa kufanyia kazi ili kupunguza mateso kwa mashabiki pamoja na wachezaji katika kutimiza majukumu yao.

    Tunaona Mashujaa wamepanda wakiwaondoa Mbeya City kwenye mchezo wa mtoano lakini kuna baadhi ya viongozi waliacha mateso kwa benchi la ufundi la Mbeya City.

    Ajabu kubwa tunaona moja ya watu wa benchi la ufundi la Mashujaa aliamua kuonyesha ushujaa wake kwa kuonekana akimpiga kocha wa Mbeya City.

    Hii sio sawa hasa kwa timu zote masuala ya kupigana uwanjani sio sawa ni muhimu kuongeza umakini na kupunguza mateso kwenye viwanja vya michezo.

    Ukiweka kando hayo ni kwenye mateso ambayo wanapitia wachezaji ambao kandarasi zao zinakaribia kufika mwisho ama mikataba yao imefika mwisho.

    Ni muda wa viongozi kuwapa taarifa ambazo zinawahusu kama wataendelea kuwa ndani ya timu ama safari itawakuta sio Yanga au Simba mpaka Geita Gold.

    Kuwapa taarifa mapema itawaongezea nguvu ya kukubali madili sehemu nyingine amayo watapata kwani maisha ya mpira lazima yaendelee.

    Tunaona wapo ambao wamepewa mkono wa asante mapema kisha kuna timu zimakamilisha mpango wa kuzipata saini zao hivyo ndivyo maisha yanakwenda.

    Mateso ni muhimu kupunguzwa kila mtu apewe haki yake inayomstahili kwa kuwa muda hausubiri.

    Previous articleKIUNGO HUYU APEWA DILI LA MIAKA MIWILI YANGA
    Next articleSIMBA MPYA USIPIME,GAMONDI NABI MTUPU