Home Sports MCHETUAJI BM HUYO SINGIDA

MCHETUAJI BM HUYO SINGIDA

MZEE wa kuchetua Bernard Morrison kiungo aliyezivuruga kwa nyakati tofauti nyavu za makipa wa Bongo akiwa mitaa miwili tofauti.

Akiwa ndani ya Yanga alimtungua Aishi Manula kwenye Kariakoo Dabi na hapo jina la mchetuaji likapatikana.

Uwezo wake ukwavutia mabosi wa Simba wakampa dili la miaka miwili akiwa huko alionyesha uwezo ikiwa ni kwenye mechi za kimataifa alizopewa nafasi.

Morrison 2021/22 akarejea kwa mara nyingine Yanga na sasa amepewa mkono wa asante akiwa ni mchezaji huru.

Ndani ya Yanga chini ya Nasreddie Nabi kwenye mechi za kimataifa alikuwa bora akitokea benchi alifanya hivyo dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini alipofunga bao katika mchezo huo.

Kwa sasa anatajwa kuwa kwenye hesabu za kuibukia Singida Big Stars ambayo inaitwa Singida Fountain Gate akaungane na mshikaji wake Pascal Wawa beki wa mpira ambaye ni nahodha pia.

Wawa uwezo anaingia kwenye orodha ya mabeki wenye uwezo mkubwa wa kupiga pasi ndefu zinazofika kwenye maeneo husika ni moja ya marafiki wa BM.

Previous articleUTAWALA WA WAGENI UTAZAMWE KWA UMAKINI
Next articleYANGA:HATUNA JAMBO DOGO