Home Sports NABI KUIBUKIA AFRIKA KUSINI

NABI KUIBUKIA AFRIKA KUSINI

BAADA ya kufikia makubaliano ya kutoongeza mkataba ñdani ya Yanga, Nasreddine Nabi anatajwa kuwa katika hesabu za Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Dili la Nabi lilikuwa linagota ukingoni mwishoni mwa msimu huu wa 2022/23.

Nabi amekiongoza kikosi cha Yanga msimu wa 2022/23 kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kutwaa taji la Ligi Kuu Bara, Ngao ya Jamii pamoja na Kombe la Azam Sports Federation.

Taarifa kutoka Yanga imeeleza kuwa wamefikia makubaliano kutoendelea na kocha huyo ambaye hajawa tayari kuendelea kuwa ndani ya kikosi hicho.

Mchezo wa mwisho Nabi kukaa benchi ilikuwa Azam FC 0-1 Yanga kwenye fainali ya Azam Sports Federation na alitwaa taji hilo.

Pia Nabi amekiongoza kikosi cha Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kugotea mshindi wa pili.

Previous articleNYOTA NTIBANZOKIZA ASEPA NA TUZO KIBAO
Next articleWAPEWA MKONO WA ASANTE AZAM FC