Home Sports NYOTA NTIBANZOKIZA ASEPA NA TUZO KIBAO

NYOTA NTIBANZOKIZA ASEPA NA TUZO KIBAO

NYOTA wa Simba Saido Ntibanzokiza amefunga msimu wa 2022/23 kabati lake likiwa limejaza tuzo sita ikiwa ni rekodi bora kwake mbele ya mastaa wa Namungo, Yanga na Singida Big Stars.

Ni Tuzo ya mchezaji bora kwa Mei akiwashinda Prince Dube wa Azam FC na Charlse Ilanfya wa Mtibwa Sugar ambapo ndani ya Mei nyota huyo alifunga mabao 7 kwenye mechi mbili alipowatungua Polisi Tanzania mabao matano na Coastal Union mabao mawili.

Juni 11 alitangazwa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuwa ni mshindi wa tuzo hiyo.

Kabla hajapoa Ntibanzokiza alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora ndani ya Simba chaguo la mashabiki kwa Mei akiwashinda Shomari Kapombe na Henock Inonga ambao aliingia nao fainali ilikuwa ni Juni 12 alipotangazwa kuwa mshindi ikiwa ni tuzo yake ya pili.

Kabati la tuzo likiwa limefungwa ghafla usiku wa Juni 12 likafunguliwa kwa mara nyingine kupokea tuzo tatu ikiwa ni tuzo ya mchezaji wa aliyeonyesha mchezo wa kiuungwana, (Fair Play).

Tuzo nyingine ya nne kusepa nayo ni ile ya kiungo bora kwa msimu wa 2022/23 akiwashinda Clatous Chama, Mzamiru Yassin ambao wapo ndani ya Simba, Bruno Gomes wa Singida Big Stars, na Aziz KI wa Yanga.

Tano ni mfungaji bora akiwa amefunga mabao 17 sawa na Fiston Mayele wa Yanga ambao wote wamesepa na tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2022/23.

Kete ya sita ambayo ni jina lake kuibukia kwenye kikosi bora msimu huu ambapo nyota huyo kibindoni ana jumla ya 12 alitoa sita akiwa Geita Gold na sita akiwa ndani ya Simba.

Previous articleMAPYA! NABI AMEANZA, MAYELE, BANGALA WANAFUATA?/ SIMBA WASHTUKA, WAMALIZA KIMYA KIMYA| KROSI
Next articleNABI KUIBUKIA AFRIKA KUSINI