Home Sports BEKI LA KAZIKAZI LASEPA NA TUZO

BEKI LA KAZIKAZI LASEPA NA TUZO

DICKSON Job beki wa kazikazi anayeitumikia Klabu ya Yanga ana tuzo ya beki bora msimu wa 2022/23.

Job wa Yanga amewashinda washkaji zake aliokuwa anapambana nao kwenye kipengele hicho ikiwa ni pamoja na nahodha wake Bakari Mwamnyeto.

Wengine ni Mohamed Hussein, Shomari Kapombe na Henock Inonga wote ni mali ya Simba.

Inonga alikuwa na tuzo hiyo msimu wa 2021/22 alipoitwaa akiwa na uzi wa Simba sasa ni shuhuda tuzo hiyo ikienda kwa watani zao wa jadi Yanga.

Ni shuhuda ya Yanga ikitwaa mataji matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na kigongo cha tatu ni Kombe la Azam Sports Federation walipopata ushindi wa 0-1 dhidi ya Azam FC.

Previous articleKIKOSI BORA SIMBA WATAWALA, SINGIDA YAPENYA
Next articleMWISHO WA UBISHI TUZO YA MFUNGAJI BORA