Home Sports MWISHO WA UBISHI TUZO YA MFUNGAJI BORA

MWISHO WA UBISHI TUZO YA MFUNGAJI BORA

KATIKA usiku wa tuzo za Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na benki ya NBC, ule ubishi wa nani atakuwa mfugaji bora uligota mwisho rasmi kwa kumtambua ambaye amesepa na tuzo hiyo.

Nyota wawili kwenye ligi walitupia mabao 17 kwa kila mmoja ikiwa ni Saido Ntibanzokoza kiungo mshambuliaji wa Simba na Fiston Mayele mshambuliaji wa Yanga.

Baada ya ligi kugota mwisho msimu wa 2022/23 Kamati ilieleza kuwa ingefanya kikao kujadili nani atatwaa tuzo hiyo kati ya nyota wa Simba ama Yanga na mwisho ubishi ukagota mwisho.

Wote wawili wamekabidhiwa tuzo zao baada ya kufunga idadi ya mabao inayolingana ambayo ni 17.

Ni Ntibanzokia ambaye ana tuzo ya kiungo bora kwa msimu wa 2022/23 ametwaa kiatu cha ufungaji bora ndani ya ligi.

Pia Fiston Mayele ametwaa tuzo yà ufungaji bora, MVP na tuzo ya bao bora ndani ya 2022/23.

Previous articleBEKI LA KAZIKAZI LASEPA NA TUZO
Next articleVIDEO:ISHU YA VIATU VIWILI VYA UFUNGAJI NAIBU AFUNGUKA