SPIKA WA BUNGE USO KWA USO NA VIONGOZI WA SIMBA

JUNI 6,2023 Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Murtaza Mangungu.

Mbali na Mangungu pia Mkurugenzi Mtendaji, Imani Kajula ni miongoni mwa viongozi waliokuwa kwenye mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Viongozi hao waliambatana Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Tawi la Simba Mjengoni, Rashid Shangazi, Makamu Mwenyekiti Tawi la Simba Mjengoni, Mhe. Hawa Mwaifunga na Katibu wa Tawi hilo Waziri Kizingiti.

Timu ya Simba inashiriki Ligi Kuu Bara na leo inatarajia kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania ikiwa ni mzunguko wa pili.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya pili huku vinara wakiwa ni Yanga ambao ni mabingwa msimu wa 2022/23.

Yanga pia wana mchezo leo dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.