MBEYA CITY 2-0 YANGA, LIGI KUU BARA

UBAO wa Uwanja wa Sokoine Mbeya unasoma Mbeya City 2-0 Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Mbeya City wameanza kwa kasi kupachika bao la kuongoza dakika ya pili kupitia kwa George Sangija.

Bao la pili limepachikwa na Richardson Ng’odya dakika ya 43 akiwa ndani ya 18.

Jitihada za mastaa wa Yanga ambao safu yao ya ushambuliaji inaongozwa na Ngushi pamoja na Clement Mzize bado hajafua dafu mbele ya Mbeya City inayopambana kutoshuka daraja.