Home Sports MTAMBO WA MABAO WAPIKWA UPYA SIMBA

MTAMBO WA MABAO WAPIKWA UPYA SIMBA

MTAMBO wa mabao ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira unaendelea kupikwa upya kwa ajili ya mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo ikiwa imegotea nafasi ya pili na pointi zake 67 ina kete mbili za kukamilisha mzunguko wa pili ndani ya ligi msimu wa 2022/23 vinara wakiwa ni Yanga.

Mbali na Yanga kuwa ni vinara wametwaa taji la ligi msimu huu wakiwa na mechi mbili mkononi.

Leo Juni 6 dhidi ya Polisi Tanzania wanatarajiwa kupambana na Simba na kigongo cha mwisho kinatarajiwa kupigwa Juni 9 dhidi ya Coastal Union na zote zitapigwa Uwanja wa Azam Complex.

Kwenye mazoezi ya mwisho Viwanja vya Mo Arena, Bunju miongoni mwa mastaa waliopo ni pamoja na Jean Baleke mwenye mabao 8 ndani ya ligi kwenye mechi 8 ambazo amecheza.

Baleke ana hat trick moja ndani ya ligi aliyowatungua Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Mbali na Baleke yupo pia Joash Onyango, Henock Inonga, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Kibu Dennis.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa maandalizi yanaendelea kwa wachezaji kwa ajili ya mechi zilizobaki.

“Tunahitaji kupata ushindi kwenye mechi zetu ambazo zimebaki na wachezaji wapo tayari kikubwa ni mashabiki kuendelea kuwa pamoja nasi na kujitokeza kwenye mechi zetu hizi za kufungia msimu,”.

Previous articleZIMETUPIA MABAO MENGI BONGO
Next articleYANGA NA SHANGWE NDANI YA MBEYA