WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA NDANI YA DAR

WAPINZANI wa Yanga kwenye mchezo wa kimataifa unaotarajiwa kuchezwa Mei 28, 2023 Uwanja wa Mkapa wamewasili ardhi ya Tanzania.

Ni alfajiri ya leo wamewasili kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

USM Alger ya Algeria ni wapinzani wa Yanga ambao watacheza fainali ya kwanza Uwanja wa Mkapa.

Saa 10:00 jioni fainali hiyo inatarajiwa kuchezwa ambapo kila timu imekuwa ikiweka wazi kuwa inahitaji kupata ushindi.

Baada ya kuwasili Bongo wachezaji wa timu hiyo waliweka wazi kuwa wanatambua upinzani uliopo na watapambana kupata matokeo chanya.