Home Sports MTIBWA SUGAR HESABU KWA KAGERA SUGAR

MTIBWA SUGAR HESABU KWA KAGERA SUGAR

IKIWA imetoka kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Polisi Tanzania tayari Mtibwa Sugar wameanza hesabu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Vinara wa ligi ni Yanga wakiwa wameshatwaa ubingwa walipokutana na Mtibwa Sugar, ubao wa Uwanja wa Manungu ulisoma Mtibwa Sugar 0-1 Yanga.

Mei 15,2023 ubao wa Uwanja wa Ushirika Moshi ulisoma Polisi Tanzania 3-1 Mtibwa Sugar na kuwafanya wapoteze pointi tatu mazima.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 14 ina pointi 29 baada ya kucheza mechi 28 itakutana na Kagera Sugar iliyo nafasi ya 7 pointi 35.

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Charles Ilanfya amesema kuwa wanafanya maandalizi kwa mechi zao zilizobaki.

“Kuna ushindani mkubwa na kila timu inahitaji kupata matokeo ambacho tunakifanya ni kuwa makini na kutumia muda tunaopata wa maandalizi kujipanga vizuri.

“Kila timu inahitaji matokeo nasi pia tunahitaji kupata ushindi kwenye mechi zetu na inawezekana,” .

Ndani ya ligi Mtibwa Sugar ikiwa imefunga mabao 28, Ilnafya katupia mabao manne.

Previous articleSIMBA KAZI INAENDELEA NAMNA HII
Next articleWAKALI WA KUTUPIA KWA KUTUMIA MGUU WA KULIA