SIMBA KAZI INAENDELEA NAMNA HII

WACHEZAJI wa Simba kesho Mei 24 wanatarajiwa kuwasili kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira na Juma Mgunda wana kazi ya kuongoza kikosi hicho kwenye mechi mbili.

Kutinga fainali kwa Yanga kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kumefanya mabadiliko hayo ndani ya ligi.

Ikumbukwe kwamba awali mchezo wa Simba dhidi ya Polisi Tanzania ulitarajiwa kuchezwa Mei 24.

Mechi mbili ambazo zimebaki mkononi mwa Simba ni mchezo dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union ambayo yote inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Kwenye mechi mbili ambazo zimebaki ni Clatous Chama atakosekana kwenye mechi hizo kutokana na rugu alilopata kwa kufungiwa mechi tatu kwa kumchezea faulo Abal Kassim wa ruvu Shooting.