AZAM FC YAIVUTIA KASI COASTAL UNION

KOCHA msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala amesema kuwa wanautazama kwa umuhimu mchezo wao ujao wa ligi baada ya kupoteza dhidi ya Namungo.

Katika mchezo uliopita Azam FC ilipoteza pointi tatu dhidi ya Namungo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ilipopoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Ongala amesema kuwa watafanyia kazi makosa ambayo yamepita kupata ushindi kwa mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union.

“Matokeo kwenye mchezo wetu uliopita hatuwezi kubadili zaidi ni kukaa na kuzungumza na wachezaji kwa ajili ya mchezo unaofuatia.

“Tunajua kwenye sehemu ambayo tulishindwa kufanya vizuri na hapo tunakwenda kufanyia kazi itoshe kusema kuwa Namungo walicheza vizuri na walistahili kupata ushindi,”.

Azam FC itacheza na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Mei 24.