YANGA HAO FAINALI, WAILIZA SINGIDA BIG STARS LITI

MFUNGAJI mwenye kasi ya hatari kuwatesa makipa ndani ya Bongo msimu wa 2022/23 amepachika bao pekee la ushindi katika hatua ya nusu fainali ya pili ya Azam Sports Federation yupo Yanga.

Anaitwa Fiston Mayele amemtungua Benedick Haule wa Singida Big Stars dakika ya 82 na kubadali usomaji wa ubao kwenye mchezo huo.

Mpaka inagotea dakika ya 90 ubao umesoma Singida Big Stars 0-1 Yanga.

Sasa Yanga inakwenda kutetea taji lake mbele ya Azam FC ambao walitangulia katika nusu fainali ya kwanza.

Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi ni Yanga ambao walitwaa taji hilo mbele ya Coastal Union ya Tanga kwenye mchezo wa fainali.

Mayele ni mshambuliaji hatari mwenye ushikaji mkubwa na nyavu.

Uwanja wa Liti kwa Singida Big Stars ni huzuni huku Yanga kwao ikiwa ni kicheko mwanzo mwisho mpaka watakapokwenda Tanga kucheza fainali.