Home Sports TUZO YA AZAM SPORTS FEDERATION SIMBA HAWAJAPENYA

TUZO YA AZAM SPORTS FEDERATION SIMBA HAWAJAPENYA

KAMATI ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzaniam (TFF) imefanya uteuzi wa washiriki katika makundi mbalimbali ya Tuzo hizo.

Ni makundi matano ambayo ni Tuzo ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation

Tuzo za Ligi Kuu ya Wanawake

Tuzo za Ligi Kuu Bara

Tuzo za Utawala

Tuzo za Ligi nyingine

Hizi ni Tuzo za Kombe la Shirikisho

Kipa Bora

Benedick Haule wa Singida Big Stars

Djigui Diarra wa Yanga

Abdulai Idrissu wa Azam FC

Mchezaji Bora

Taarifa imeeleza kuwa wateule watatangazwa Mei 21 baada ya mechi ya nusu fainali ya pili kati ya Singida Big Stars dhidi ya Yanga

Mfungaji bora ambapo mshindi ni yule atakayekuwa amefunga mabao mengi

Andrew Simchimba wa Ihefu katupia mabao 7 lakini timu hiyo imeondolewa kwenye mashindano ila mabao hayajafutwa

Clement Mzize wa Yanga katupia mabao sita

Abdul Suleiman wa Azam katupia mabao matatu.

Katika orodha hii hakuna nyota kutoka kikosi cha Simba ambaye amepenya .

Previous articleVIDEO:AMBANGILE AFUNGUKIA ISHU YA AHMED ALLY
Next articleTUZO LIGI KUU BARA KIVUMBI TUPU,PILATO WA SIMBA V YANGA NDANI