YANGA KAZI BADO HAIJAGOTA MWISHO

    USIOGOPE  kukabiliana na magumu kwa kuwa yanakukomaza uwe imara zaidi hivyo itakuwa hivyo kwa wawakilishi wa Tanzania Yanga kwenye anga la kimataifa.

    Ushindi wa mchezo wa kwanza haina maana kwamba kazi imegota mwisho bado kuna safari nyingine kukamilisha mwendo wa kuifuata fainali.

    Nyumbani ilikuwa furaha kwa kuwa kila mmoja aliona namna wachezaji walivyocheza kwa kujituma kusaka ushinda na mwisho ikawa hivyo.

    Nusu fainali ya kwanza majalada yake tayari yameshafungwa na sasa yanafunguliwa majalada ya nusu fainali ya pili.

    Hatua nyingine kubwa na ngumu kwa Yanga ambayo inapambania kutinga hatua ya fainali.

    Kama iliwezekana kupata ushindi nyumbani ina maana kwamba hata ugenini inawezekana lakini ukweli ni kwamba kazi sio nyepesi.

    Ili kazi iwe nyepesi ni lazima kila mchezaji kutimiza majukumu yake kwa umakini na kushirikiana kwenye  kila idara.

    Kuanzia ulinzi na ushambuliaji ni kazi moja kuhakikisha matokeo yanapatikana.

    Sio ushambuliaji tu hata viungo nao wanapaswa kutimiza majukumu kwa umakini kwa kuwa kazi ya kuelekea fainali inaihusu timu na sio mchezaji mmoja.

    Ipo wazi kwamba mchezaji anashinda rekodi zake binafsi lakini timu inashinda mataji hivyo ni muhimu kuendelea kucheza kwa ushirikiano ndani ya uwanja.

    Kwa wale mashabiki ambao watajitokeza uwanjani ni muhimu kupambana kwenye ushangiliaji ili kuongeza nguvu kwa wachezaji kusaka ushindi.

    Kila la kheri Yanga ni wakati wa kazi na inawezekana kupata ushindi ikiwa mtajituma kwa hali na mali.

    Previous articleNABI KUWASHANGAZA MARUMO, HAWA HAPA KUKOSEKANA
    Next articleWAKALI WA PASI ZA MWISHO BONGO HAWA HAPA