NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amepanga kuwashangaza wapinzani wake Marumo Gallants kutokana na mpango kazi atakaotumia kwenye mchezo huo kuwa tofauti na ule wa awali.
Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 2-0 Gallants na mabao yakifungwa na Aziz KI na Bernard Morrison.
Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa kutakuwa na mabadiliko kwenye kikosi kwa kuna mchezaji aliyecheza hatakuwepo kutokana na sababu maalumu.
“Mchezo wetu wa nusu fainali ya pili ni muhimu kupata ushindi tuna amini kuwa benchi la ufundi chini ya kocha Nabi, (Nasreddine) watakuwa na jambo litakalowashangaza kwani Bernard Morrison atakosekana hivyo kutakuwa na mwingine ambaye atakuwa kwenye nafasi hiyo.
“Mbali na kumkosa Morrison bado kipa wetu Aboutwalib Mshery naye hajawa fiti hawa wamebaki Dar lakini tumeungana na Dennis Nkane ambaye hakuwa kwenye misafara iliyopita hivyo tunaamini kila kitu kitakwenda sawa,”.
Yanga inatarajia kucheza mchezo wa hatua ya nusu fainali ukiwa ni mchezo wa pili na mshindi wa jumla atatinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.