BANDA KAJENGA KIBANDA NDANI YA MSIMBAZI

KIUNGO wa Simba Peter Banda ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 amejenga kibanda chake mwenyewe kwa kushindwa kuonyesha makeke yake ndani ya uwanja.

Moja ya sababu kubwa iliyofanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu ni kupambania hali yake kutokana na kutokuwa fiti kwa muda mrefu.

Banda hana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza licha ya kurejea kwenye ubora wake na amekutana na ugumu kwenye kutengeneza nafasi za kufunga wala kufunga mabao.

Kagotea kwenye bao moja pekee ambalo alifunga dhidi ya Singida Big Stars.

Katika mchezo huo alitokea benchi na kufunga na bahati mbaya tena akaumia akawa nje ya uwanja kwa muda mwingine tena.

Bao ambalo alifunga Banda lilitosha kufanya ubao wa Uwanja wa Liti kusoma Singida Big Stars 1-1 Simba na wababe hao wakagawana pointi mojamoja.

Kwenye mechi za hivi karibuni ameanza kupewa nafasi lakini bado hajaonyesha ukomavu wake ndani ya uwanja ni muhimu kwake kujituma zaidi kama atabaki katika kikosi cha Simba msimu ujao.