HONGERENI YANGA, KAZI BADO HAIJAGOTA MWISHO

YALE ambayo yalipangwa kwa kila mmoja kwenye msimu wa 2022/23 taratibu wengine wameshakamilisha na wengine bado wanasubiri mpaka mwisho.

Ruvu Shooting ni mwendo wameumaliza kwenye mechi za ligi baada ya kushuka ndani ya ligi na sasa wanaibukia Championship.

Wale ambao wamekwama kufikia malengo yao wakiwa wanasubiria mechi mbili za mwisho ni lazima wapambane kufikia malengo yao waliyofikiria.

Kila timu inatambua kazi kubwa ipo kwenye kutimiza malengo na pale ambapo walikwama kupambana kusaka pointi tatu wakashindwa basi kazi iendelee.

Hongereni Yanga kwa kutwaa ubingwa na imekuwa hivyo kama ambavyo mlifanya msimu uliopita hii ni kubwa kwenu na kila mmoja lazima afurahie mafanikio hayo.

Hakuna kitu chepesi kwenye kufikia mafaniki na kazi ambayo inafuata kwa sasa ni kuendeleza mazuri ambayo yalifanywa kwa msimu huu na kuanza kazi kwa wakati ujao.

Ni moja ya msimu ambao umekuwa bora kwa Yanga kutokana na kazi kubwa inayofanywa na wachezaji ndani ya uwanja.

Ruvu Shooting kuangukia Championship sio bahati mbaya bali kuna mahali walikwama hivyo ni muhimu kuchukua yale walyokesea ili kuwa imara wakati ujao.

Kwa zile ambazo zitabaki na kucheza ndani ya ligi ni muhimu kufanya kazi kubwa kwa ajili ya msimu mpya ujao.

Kila mmoja anatambua namna ya kufanya na kila mchezaji ni muhimu kushinda mechi ambazo zimebaki na kukamilisha kwa umakini mzunguko wa pili