Home Sports HIKI NDICHO WANACHOKITAKA SIMBA

HIKI NDICHO WANACHOKITAKA SIMBA

NAHODHA wa Simba John Bocco, amesema kuwa kwa sasa wanatafuta heshima pekee ya kukamilisha ligi na ushindi kwenye mechi zote mbili zilizobakia ili kurejesha furaha kwa mashabiki wao.

Tayari mabingwa wa ligi ni Yanga wanaonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia wakiwa na pointi 74.

Ijumaa iliyopita Simba iliishusha rasmi Ruvu Shooting kwa kuichapa mbao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

 Bocco amesema nia yao kwa sasa kuhakikisha mechi mbili zilizobaki wanashinda ili kuendeleza heshima yao.

“Kila mchezaji hajapenda haya yalitokea tuna amini kwamba ni muda wa kuwapa furaha mashabaki wetu kwenye mechi zetu ambazo zimebaki.

“Umuhimu wa mechi zilizosalia kwetu naweza kusema wazi kuwa hizi mechi ni za kutufariji baada ya kukosa makombe mengi hivyo tunahitaji pointi zote katika kila mchezo ili tumalize ligi kwa furaha,” amesema Bocco.

Previous articleHONGERENI YANGA, KAZI BADO HAIJAGOTA MWISHO
Next articleWAMEKWISHA, WACHEZAJI YANGA WAFANYA KIKAO, ROB ATAJA ‘MCHAWI’