JURGEN Klopp Kocha Mkuu wa Liverpool ameshuhudia vijana wake wakivuja jasho dakika 90 mbele ya Spurs.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Anfield umesoma Liverpool 4-3 Spurs.
Liverpool walianza kupachika bao dakika ya 3 kupitia kwa Curtin Jones kisha dakika ya 5 Luis Diaz alipiga msumari wa pili na Mohamed Salah dakika ya 15 Kwa mkwaju wa penalti.
Dakika ya 39 Hary Kane alipachika bao la Kwanza, Son Heung-min dakika ya 77 na Richarlison dakika ya 90+3.
Bao la ushindi ni mali ya Diogo Jota dakika ya 90+4