Home Sports AZAM FC MACHO YOTE NUSU FAINALI

AZAM FC MACHO YOTE NUSU FAINALI

KALI Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema mchezo wao wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba ni muhimu kupata ushindi ili wasonge mbele hatua inayofuata.

Ni nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 6,2023 Uwanja wa Nangwanda,Mtwara.Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Ni ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ilipata wakati Simba ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 5-1 Ihefu mechi zote zilichezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ongala amesema kila timu inahitaji ushindi hivyo watafanya maandalizi mazuri.

“Mchezo wetu dhidi ya Simba hautakuwa mwepesi ipo wazi kwani kila timu inahitaji ushindi nasi tunafanya maandalizi kwa mechi ijayo kupata matokeo mazuri.

“Ushindi wetu dhidi ya Ruvu Shooting umetupa nguvu kwa ajili ya mechi hiyo kwani vijana walicheza vizuri na kupata matokeo hivyo ni kazi kwetu kuendelea pale ambapo tuliishia,”

Previous articleVIDEO:NYAMBAYA ATOBOA SIRI YANGA KUCHEZA FAINALI
Next articleSIMBA YATAMBIA MFUMO WAKE